1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Kabila aelekea kushinda uchaguzi wa rais

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsv

Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo rais anayetetea wadhifa wake Joseph Kabila inaonekana anaelekea kushinda marudio ya uchaguzi wa rais wakati kura zote zikiwa karibu zimemalizika kuhesabiwa.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali kuongoza kwa Kabila dhidi ya mpinzani wake mkuu Jean- Piere Bemba kunaonekana kwamba hakuwezi kupikuliwa.Uchaguzi huo ni wa kwanza kufuatia mgogoro wa miaka mitano katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Hali ya mvutano bado ingalipo katika mji mkuu wa Kinshasa kufuatia mapambano ya silaha mwishoni mwa juma kati ya vikosi vya wagombea hao wawili.

Wakati huo huo polisi imewakamata zaidi ya watu 300 wasiokuwa na makaazi wakiwemo watoto wengi wazururaji kwa kuwalaumu kuanzisha vurugu hizo.