1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Kabila na Bemba wamekubali kujadiliana

27 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDHm

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mpinzani wake mkuu wa kisiasa,makamu wa rais Jean Pierre Bemba,wamekubali kukutana kwa majadiliano,baada ya nchi hiyo kushuhudia ghasia za juma moja.Wanasiasa hao wawili mwezi wa Oktoba,watakumbana tena katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Hadi watu 23 waliuawa katika machafuko yaliyotokea baada ya kutangazwa,hakuna mshindi wa moja kwa moja aliepatikana,katika duru ya mwanzo ya uchaguzi.Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa wanasiasa wote wawili kuonyesha uvumilivu wakijitayarisha kwa duru ya pili ya uchaguzi.Kwa hivi sasa,vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Kinshasa,vinasimamia makubaliano ya kuacha mapigano.