1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Kabila na Bemba watapambana duru ya pili

21 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJX

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo atapambana tena na kiongozi wa zamani wa waasi,Jean-Pierre Bemba katika duru ya pili ya uchaguzi,mwezi wa Oktoba.Tume huru ya uchaguzi nchini Kongo imetangaza hayo baada ya wagombea hao wawili kukosa kufikia kiwango cha asilimia 50 kilichohitajika ili kupata ushindi wa moja kwa moja.Rais Kabila amepata asilimia 45,huku mpinzani wake bwana Bemba akiwa na asilimia 20 pekee.Kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, askari mmoja,mfuasi wa Bemba,aliuawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa rais Kabila,baada ya vurugu kuzuka karibu na ofisi ya tume ya uchaguzi katika mji mkuu Kinshasa.