1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Majeshi ya Ujerumani kuondoka DRC.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnl

Majeshi ya Ujerumani yako njiani kurejea nyumbani kutoka katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo baada ya kukamilisha ujumbe wao wa kulinda amani katika jeshi la umoja wa Ulaya wakati wa uchaguzi wa hivi karibuni wa rais na wabunge.

Wizara ya ulinzi mjini Berlin imesema ujumbe huo wa kulinda amani umefanikiwa kusaidia kuleta amani ambapo upigaji kura ilifanyika kwa amani. Wanajeshi 780 wataondoka mjini Kinshasa pamoja na mji mkuu wa Gabon , Libreville katika muda wa siku chache zijazo ili kuweza kuwa nyumbani wakati wa sherehe za sikukuu ya Krismas.

Sherehe za kuwaaga wanajeshi hao zinatarajiwa kufanyika leo mjini Kinshasa.