1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yaonyesha Kabila anaongoza

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt2

Majuma mawili baada ya kufanywa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na baada ya takriban kura zote kuhesabiwa inadhihirika kuwa rais wa hivi sasa Joseph Kabila anaongoza kwa kama asilimia 60.Kwa upande mwingine mpinzani wake Jean-Pierre Bemba alie makamu wa rais,amejinyakulia asilimia 40 ya kura zilizohesabiwa.Hayo ni kwa mujibu wa halmshauri huru ya uchaguzi.Mwisho wa juma lililopita wafuasi wa Kabila na Bemba walipambana mjini Kinshasa.Watu wanne waliuawa katika machafuko hayo.