KINSHASA: mseto wa Kabila uchaguzi wa bunge nchini JKK
10 Septemba 2006Matangazo
Mseto unaomwuunga mkono rais Joseph Kabila umeshinda katika uchaguzi wa bunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Uchaguzi huo uliofanyika mnamo mwezi Julai ulikuwa wa kwanza kuitishwa katika nchi hiyo baada ya miaka 40.
Hatahivyo raundi ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika mwishoni mwa mwezi oktoba ambapo rais wa sasa bwana Kabila atapambana na makamu wake Jean Pierra Bemba.