KINSHASA: Rais Joseph Kabila, atoa mwito wa utulivu
17 Novemba 2006Matangazo
Rais wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila ametoa mwito wa utulivu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita. Tume huru ya uchaguzi ilitangaza kuwa rais Kabila alipata ushindi na asili mia 58 ya kura huku mpinzani wake Jean Pierre Bemba akipata asili mia 42.
Bemba alipinga matokeo hayo na kudai kwamba atatumia kila njia halali kuyapinga matokeo hayo.
Wachunguzi wa kimataifa ambao walifuatilia uchaguzi huo wa nchini Congo wanasema kwa jumla uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, lakini wafuasi wa Bemba wanasema uchaguzi huo ulikuwa na hitilafu.
Itabidi matokeo hayo yaidhinishwe na korti kuu ya taifa kabla ya rais Kabila kuweza kuyapishwa tarehe 10 mwezi ujao.