1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wafuasi wa Kabila na Bemba wamefyatuliana risasi

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtl

Risasi zimefyatuliwa kati ya wafuasi wa wagombea urais wawili katika mji mkuu Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wanajeshi wanaomuunga mkono makamu wa rais Jean-Pierre Bemba wamesema kuwa wamepambana na polisi walio watiifu kwa rais Joseph Kabila.Wanajeshi wa Kifaransa wa Umoja wa Ulaya na vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vimekaa macho.Matokeo kamili ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais,iliyofanywa tarehe 29 Oktoba bado hayakutangazwa,lakini kundi la Bemba limeshadai kuwa kulikuwepo utaratibu wa udanganyifu.Baadhi ya matokeo yaliotolewa na wanadiplomasia na wataalamu wa uchaguzi huonyesha kuwa Kabila anaongoza.Kwa mujibu wa maripota, wakazi wa Kinshasa wanamuunga mkono Bemba.Baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi hapo mwezi wa Agosti,vikosi vilivyo tiifu kwa wagombea urais wawili vilipambana mjini Kinshasa.Katika mapambano hayo,si chini ya watu 23 walipoteza maisha yao.