KINSHASA:Bemba atafuta hifadhi kwenye ubalozi wa Afrika Kusini
23 Machi 2007Matangazo
Mwanasheria mkuu nchini Kongo ametoa hati ya kukamatwa kwa Seneta Jean Pierre Bemba kufuatia ghasia kutokea hapo jana mjini Kinshasa.Bwana Bemba anaripotiwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa nchi ya kigeni huku mapigano yakiendelea.Kulingana na mwanasheria Mkuu Tsaimanga Mukenda kinga aliyo nayo kwasababu ya kuwa Seneta au kujificha katika ubalozi huo wa kigeni hakumzuii kutokamatwa.Milio ya risasi inaripotiwa kuendelea kusikika na mali kuporwa.
Mapigano yalizuka hapo jana baada ya wafuasi wa Jean Pierre Bemba kiongozi wa upinzani kupambana na majeshi ya serikali mjini Kinshasa.