1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Chama cha Kabila chaongoza uchaguzi wa bunge.

8 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEQ

Chama chaVugu vugu la kisiasa cha rais anaemaliza wadhifa wake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila kimeongoza matokeo ya uchaguzi wa Bunge wa July 30 iliyopita.

Hayo ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa usiku wa kuamkia leo na kamisheni huru ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa kamisheni hiyo, chama cha vugu vugu la kisiasa AMP cha rais Kabila kimepata zaidi ya viti 200 toka jumla ya viti mia tano vya bunge jipya la taifa, nafasi ya pili inashikiliwa na muungano wa wazalendo wa Kongo wa (renako), unaomuunga mkono makamo wa rais Jean Piere Bemba kilichojipatia viti 100 hadi sasa.

Bunge jipya linatazamiwa kukutana baada ya siku kumi tano kuanzia hivi sasa.