Kinshasa:Khaofu ya machafuko yatanda DRC.
22 Agosti 2006Matangazo
Kwa mara ya kwanza vikosi vya kijeshi vya Umoja wa Ulaya vinavyosimamia uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimechukua hatua baada ya kutokea ghasia.
Baada ya miripuko ya risasi iliyowalazimisha maafisa wa Umoja wa Mataifa na mabalozi waliokwenda kumtembelea mgombea urais Jean-Pierre Bemba kubakia kama mahabusu ndani ya nyumba ya mgombea huyo.
Kiasi cha wanajeshi 150 wa Hispania wameungana na vikosi vya Umoja wa Mataifa kuenda kutoa msaada kwa mabalozi hao.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema, wanajeshi wanaomtii rais Joseph Kabila walishambulia makaazi yaraia huko Kinshasa.
Kabila na Bemba wanatazamiwa kuingia katika hatua ya pili ya uchaguzi hapo October 29, baada ya matokeo ya uchaguzi uliyopita kushindwa kutoa mshindi.