1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Mtoto wa Mobutu ataka kumuunga mkono Kabila.

11 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDb

Mtoto wa kiume wa rais wa zamani wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Mobutu Sese Seko amesema jana Jumapili kuwa anajadili uwezekano wa kupata makubaliano yatakayosaidia rais Joseph Kabila kushinda uchaguzi wa duru ya pili mwezi Oktoba.

Msaada huo unaweza kumsaidia Kabila kujenga kiungo imara kuunganisha mgawanyiko uliopo sasa kati ya upande wa mashariki na magharibi nchini humo.

Francois Joseph Mobutu Nzanga ambaye alishiriki katika uchaguzi mkuu nchini humo na kumaliza akiwa katika nafasi ya nne , kutokana na kuungwa mkono zaidi katika eneo la magharibi hasa katika jimbo la Equatorial.

Wakati huo huo mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana anatarajiwa kuizuru jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo leo Jumatatu na Jumanne na anapanga kukutana na mahasimu wawili katika uchaguzi mkuu uliopita rais wa sasa Joseph Kabila na makamu wa rais Jean-Pierre Bemba.