1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Muungano wa Kabila waongoza uchaguzi wa Bunge.

4 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFR

Kwa mujibu wa matokeo ya hadi hivi sasa kundi la vyama linaloongozwa na rais Joseph Kabila wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaongoza katika uchaguzi wa bunge.

Kufuatia matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi Muungano wa vyama 31 vinavyomuunga mkono rais Kabila, umepata viti 169 kati ya viti 340 kura ambazo zimeshahesabiwa, huku chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na Jean-Pierre Bemba kikipata viti 47.

Kwa mujibu wa uchaguzi huo kuna jumla ya viti mia tano vya uwakilishi bungeni ambavyo vinagombaniwa katika nchi hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aidha uchaguzi huo umekuwa ni hatua moja wapo ya maendeleo ya kisiasa baada ya umwagaji wa damu uliodumu kwa miaka mitano katika nchi hiyo ya Afrika ya kati na ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika baada ya miaka 46 nchini humo.