1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kibiashara atiwa mbaroni Korea ya Kusini

10 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkU
SEOUL: Nchini Korea ya Kusini ametiwa mbaroni mkuu wa kampuni ya tatu kubwa ya kibiashara wa Kundi la SK nchini humo pamoja na wabunge sita. Wabunge hao wanashutumiwa kupokea pesa za ulipaji rushwa kutoka makampuni ya kundi hilo la kibiashara na kukiuka sheria ya vyama vya kisiasa ya nchi. Mwenye Kiti huyo wa Kundi la SK, Son Kil Seung anakabiliwa na shutuma ya kutolipa kodi na kuiba pesa za kampuni. Nao upinzani unamlaumu mtoa mashtaka mkuu wa serikali kuwatia mbaroni viongozi hao ili kukandamiza ukweli wa kuhusika Rais Roh Moo Hyun katika orodha ya kashfa za ulaji rushwa.