Urrutia aapa kuzuia sherehe za kumuapisha Maduro Venezuela
7 Januari 2025Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, Gonzalez Urrutia, ameapa kuondowa kile alichokiita kuwa khofu, na kuzuia mipango ya Nicolas Maduro ya kuapishwa madarakani kwa muhula mwingine.
Kiongozi huyo wa upinzani aliyekimbilia uhamishoni, ametowa mwito wa kufanyika maandamano makubwa pamoja huku hapo jana akiitembelea ikulu ya White House kutafuta uungwaji mkono wa kimataifa.
Soma pia: Marekani yamtambua Gonzalez Urrutia kama rais mteule wa Venezuela
Alikutana na rais wa Marekani anayeondoka,Joe Biden katika juhudi zake za mwisho za kumshinikiza Maduro aachie madaraka.
Nicolas Maduro mwenye umri wa miaka 62 aliyeitawala Venezuela kwa zaidi ya muongo mmoja tangu kifo cha mtangulizi wake Hugo Chavez, ataapishwa Ijumaa kuongoza muhula wa tatu wa miaka sita.
Upinzani umedai uchaguzi wa Julai ulikumbwa na udanganyifu na wizi wa kura.