SiasaMsumbiji
Mkuu wa upinzani Msumbiji arejea nchini kutoka uhamishoni
9 Januari 2025Matangazo
Mondlane aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais, alionekana akishuka kutoka kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Mavalane, ulioko kwenye mji mkuu, Maputo.
Kiongozi huyo wa upinzani aliondoka nchini humo mwezi Oktoba baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata na kusababisha maandamano makubwa ya vurugu yalioitumbukiza nchi hiyo katika mzozo.
Amesema aliondoka nchini humo kwa kuhofia usalama wa maisha yake baada ya wanachama wawili waandamizi wa chama chake cha upinzani kuuawa na watu wasiojulikana mara tu baada ya uchaguzi.