Ukraine imesema imemuuwa afisa mwandamizi katika jeshi la Urusi Jenerali Igor Kirillov, kwa kutumia bomu lililokuwa limetegwa nje ya nyumba moja ya makaazi. Sasa kuuwawa kwa Kirillov ni pigo kwa kiasi gani kwa Urusi? Swali hilo na mengine Jacob Safari amemuuliza mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka mjini Cologne, Ujerumani, ambaye pia alikuwa mhariri mkuu wa DW Mohammed Abdul-Rahman.