1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiptum aivunja rekodi ya London Marathon

24 Aprili 2023

Mkenya Kelvin Kiptum hapo Jumapili aliweka rekodi katika mbio za London Marathon alipokimbia kwa muda wa saa mbili, dakika moja na sekunde ishirini na tano.

https://p.dw.com/p/4QUFa
England | London Marathon 2021
Picha: Rob Pinney/Getty Images

Kiptum licha ya kuweka rekodi anakuwa mtu wa pili duniani kukimbia marathon kwa muda wa saa mbili na chini ya dakika mbili baada ya Eliud Kipchoge ambaye anashikilia rekodi ya dunia.

Eliud Kipchoge gewinnt Berlin Marathon
Eliud Kipchoge akishiriki mbio za Berlin MarathonPicha: imago images

"Nafurahia sana kukimbia kwa muda wa pili kwa kasi katika historia. Maandalizi yangu yalikuwa mazuri na kila kitu kilikwenda vizuri. Kuivunja rekodi ya dunia, kwa sasa sijafikiria labda nikifika nyumbani nitalifikiria hilo," alisema Kiptum.