Kocha wa Bremen azungumzia hali tete ya kifedha klabuni
8 Oktoba 2020Klaassen amerejea katika klabu ya Ajax Amsterdam katika siku ya mwisho ya uhamisho siku ya Jumatatu kwa kitita cha euro milioni 11. Pia wanalenga kumuuza Milot Rashica kwa Bayer Leverkusen hali ambayo hata hivyo haikuweza kufanikiwa.
"Hatujafikia lengo letu la uhamisho kwa mtazamo wetu wa kispoti, " Kohfeldt amesema baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya St Pauli Hamburg, usiku wa Jumatano.
"Lakini Werder Bremen imo katika hali mbaya ya kifedha. Kila mmoja ni lazima atambue hilo, na kila mmoja ni lazima apambane."
Maingwa hao wa zamani wa Bundesliga wameathirika pakubwa na janga la virusi vya corona na uwanjani waliepuka tu kushuka daraja msimu uliopita katika mpambano wa mchujo dhidi ya timu ya daraja la pili.
Wameanza msimu mpya kwa ushindi mara mbili kutoka michezo mitatu lakini Kohfeldt alisema wanapaswa kuimarika "kutokana na hali ya juu ya kitisho" katika michezo.