Kombe la BDF Bayern yaingia kwa kishindo robofainali
23 Desemba 2010Bayern ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo la DFB ilivurumisha VfB Stuttgart, kwa mabao 6-3, ambapo Miroslav Klose alipachika mabao 2 kati ya hayo.
Bayern sasa katika robofainali itapambana na Alemannia Aachen ambayo iliipiga kumbo Eintracht Frankfurt katika mechi iliyoamuliwa kwa changamoto ya penalti, baada ya kuwa sare ya bao 1-1 hadi mpambano ulipoisha.Aachen walitumbukiza penalti nne wakati Frankfurt walipata mbili.
Nayo timu ya daraja la pili Energie Cottbus, iliwaaibisha VfL Wolfsburg inayoshiriki katika Bundesliga kwa kuichapa mabao 3-1 na kufuzu kwa robofainali.Cottbus sasa itapambana na Hoffenheim katika robofainali.
Timu nyingine ya Bundesliga FC Cologne iliadhiriwa na timu ya daraja la pili Duisburg kwa kuchapwa mabao 2-1 na kusukumizwa nje ya michuano hiyo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo