1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia:Brazil yaichapa Korea Kaskazini

Mtullya Abdu16 Juni 2010

Katika mashindano ya kugonbea kombe la dunia nchini Afrika kusini, Brazil iliichapa Korea ya Kaskazini mabao 2 kwa moja.

https://p.dw.com/p/Nrra
Mchezaji maaruf wa Brazil Kaka na mwenzake Robinho.Picha: picture-alliance/dpa

Katika mechi zingine Ivory Coast na Ureno ziitoka bila kwa bila, na New Zealand ilirudisha goli katika dakika za mwisho na kutoka sare na Slovakia-bao moja kwa moja.

Leo Honduras itapambana na Chile. Uhispania itacheza na Uswis na mwenyeji wa mashindano Afrika Kusini itaingia tena uwanjani kuchuana na Uruguay.