KOMBE LA KLABU BINGWA ULAYA NA AFRIKA
11 Aprili 2005LIGI MASHUHURI BARANI ULAYA-REAL YAJA JUU DHIDI YA FC BARCELONA
CHAMPIONS LEAGUE-BAYERN MUNICH YAISUBIRI KESHO CHELSEA NA
KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA
Tukianza na Bundesliga-ligi ya ujerumani,Bayern Munich iliokua bega kwa bega na sxchalke pointi 56 kila moja, ilifungua mwanya wa pointi 3 mwishoni mwa wiki baada ya kuizaba Borussia Moenchengladbach mabao 2:1.Munich ilipata msaada wa jirani zao Stuttgart waliowakandika mahasimu wao Schalke mabao 3-0.
Zikisalia mechi 6 tu kabla msimu kumalizika, Munich inaongoza Ligi ya Ujerumani kwa pointi 59 ikifuatwa na schalke yenye pointi 56.
Stuttgart ilioparamia ngazi ya Ligi hadi nafasi ya 3,iliizidi nguvu Schalke pale mshambulizi wao Kevin Kuranyi alipolifumania lango la Schalke mara 3 .
Stuttgart sasa ina jumla ya pointi 54 na ina nafasi pia kama Schalke na Munich kutawazwa mabingwa msimu huu.
Katika Ligi ya Spain, Real Madrid ilirudi kutamba baada ya mabao ya majogoo wake 3:Zinedine Zidane,Raul na Ronaldo.Real iliizaba FC barcelona mabao 4:2 na sasa Real inaweza kutarajia tena kutwaa taji.,
Barcelona sio tu ilipatwa na pigo hilo la kushindwa, bali mshambulizi wake Samuel Eto’o kutoka Kamerun ameumia goti.Eto’o ndie anaeongoza orodha ya watiaji magoli katika la Liga –ligi ya Spain.
Hatahivyo, bao la Ronaldinho,katika lango la Real lilikua maridadi ajabu kutoka mkwaju wa free-kick ambao ulimhadaa kipa wa Real Iker Casillas.
Katika Ligi ya Itali-Sirie A, viongozi wa Ligi AC Milan na Juventus inayosimama nafasi ya pili zilitoka suluhu na maadui zao ingawa kwa njia tofauti. Katika changamoto na Florence,Juventus iliotoka nayo nyuma na kutoka sare 3:3 na Fiorentina. AC Milan hatahivyo inaongoza Ligi ya itali kwa magoli.
Katika Premier League-Chelsea ambayo ina miadi kesho na viongozi wa Ligi ya Ujerumani katika robo-finali ya Champions League-ilikuwa imeshazabwa bao 1:0 na Birmingham City.Lakini zikisalia dakika 8 tu,Muivory Coast Didier Drogba akaipatia Chelsea bao la kusawazisha.Hatahivyo, Chelsea imeungan’ganaia usukani wa Ligi ikiwa pointi 11 mbele ya Arsenal inayosimama nafasi ya pili.Manchester iko pointi 14 nyuma ya Chelsea.
CHAMPIONS LEAGUE:
Kesho itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu,atie gongo-mkutano katika Uwanja wa olimpik wa Munich:
Itaamuliwa kesho ni timu gani 4 bora zitaingia nusu-finali ya Chamipions League:Bayern Munich inajiwinda kuingia nyumbani kesho ikicheza na Roy Makaay na Claudio Pizzaro kufuatamabao 2: iliochapwa zaidi na Chelsea-viongozi wa Ligi ya Uingereza.
Chelsea aliefungiwa.Hatahivyo, Chelsea inapigiwa tena upatu kuitoa Munich nje ya Champions League kufuatia ushindi wao wa duru ya kwanza wa mabao 4:2.Lilikua bao la dakika za mwisho za kufidia la mkwaju wa penalty lililofufua matumaini ya Munich ama sihivyo, wangekuwa wameshazikwa huko London wiki iliopita.
KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:
mabingwa watetzezi Enyimba walipiga hatua kubwa mwishoni mwa wiki kuingia duru ijayo ya Kombe hili baada ya kuitimua jana Red Arrows ya Zambia kwa mabao 3:0 mjini Aba.
Enyimba waliotwaa Kombe hilo la klabu bingwa kwa mara ya pili mfululizo desemba mwaka jana, wanaelekea nao watakata tiketi nyengine ya awamu ya pili ya Kombe hilo.Klabu nyengine ya Nigeria Dolphin FC pia imenyakua ushindi wa mabao 2:0 dhidiya ASEC Abidjan m jini Port Hercourt.
Mabingwa wa zamani wa Afrika Raja Casablanca ya Morocco walisawazisha dakika za mwisho mjini Abidjan wakati wa changamoto yao na Africa Sports.
Waakilishi wengine wa Morocco-Royal Armed Forces walishinda bao 1:0 nyumbani mwa Etoile du Sahel ya Tunisia kufuatia mkwaju wa penalty .Etoile ndio makamo-bingwa wa Afrika.
Ajax Cape Town iliichapa klabu isio mashuhuri ya Fello Star Labe ya Guinea kwa mabao 2:0.
Mjini Luanda, AS Aviacao ya Angola ilitoka suluhu bao 1:1 na Zamalek ya misri wakati Esperence ya Tunisia ilichapa Kaizer Chief ya Afrika kusini mabao 4:0.