1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la klabu bingwa Ulaya

5 Machi 2008

Schalke ina miadi na FC porto leo wakati jana Arsenal london iliivua taji AC milan ya Itali.

https://p.dw.com/p/DJ2E

Duruy a kwanza ya kutoana ya champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya inaendelea leo baada ya jana Arsenal London kuwavua taji mabingwa FC Milan ya Itali uwanjani mwao San Siro.

Jioni hii waakilishi pekee wa Bundesliga-ligi ya ujerumani Schalke wana miadi huko Ureno na FC Porto wakati Chelsea ya Uingereza wamepania nyumbani na akina Didier Drogba kuwaadhibu Olympiakos ya Ugiriki baada ya kuachana suluhu 0:0 duru iliopita.Chelsea inataka kufuata nyayo ya Manchester United ilioitoa jana Lyon ya Ufaransa.

Real Madrid ya Spian wanawakaribisha AS Roma ya Itali ambayo baada ya kutimuliwa AC Milana na Kaka wao,wanapepea bendera ya Italy katika kinyan’ganyiro hiki.

Schalke, waakilishi pekee wa Ujerumani katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya wanakumbana na FC Porto ya Ureno-mabingwa wa zamani wakijua kwamba hatima yao katika kombe hili yaweza ikyaamuliwa leo .Schalke imekuwa ikipepesuka karibuni na hasa baada ya kuzabwa bao 1:0 nyumbani hapo jumamosi.Isitoshe, wakati FC Porto chini ya Mourinho iliwahi kutawazwa mabingwa wa champions League,Schalke haikuwahi kuvuka kizingiti cha robo-finali ya kombe hili.

Mabingwa mara 9 wa ulaya Real Madrid ya Spain yamkini sana ikacheza leo bila ya jogoo lao la Holland Ruud van Nistelrooy inapopania kufuta mabao 2-1 lao la duru ya kwanza kati yake na wataliana AS Roma.

Van Niestelrooy ameumia goti na kocha wake mjerumani bernd Schüster amearifu kwamba kwa uhakika hatateremka leo uwanjani.

Chelsea ya Uingereza inabidi kunoa mizinga yake usoni ya akina Didier Drogba na Michael Essien ni mikali tena ,kwani wenzao Arsenal na Manchester wamekwishatamba hapo jana .Chelsea baada ya kumudu sare ya 0:0 na Olympiakos mjini Athens, ni zamu yake leo kutamba nyumbani mjini London.Jumamosi mizinga ya Chelsea ilionesha ukali wake ilipoihilikisha West Ham kwa mabao 4:0 katika pirika pirika za premier League.Matumaini ya wagiriki kuitimua leo Chelsea nyumbani mwao yamepata mkosi kwa kuumia simba wao wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Lomana LuaLua.

Chelsea imekua ikitamba katika mechi zake 5 zilizopita za kombe hili la ulaya wakati Olympiakos imekuwa ikilazwa si kwa chini ya mabao 2 kila ilipozuru London mara 7 zilizopita.

Jana Arsenal London, ilifanya mojawapo ya miujiza mikubwa ya dimba chini ya kocha wao mfaransa Arsene Wenger walipowavua taji nyumbani mwao mabingwa AC Milan ya Itali na kuwatoa nje ya kinyan’ganyiro hiki kwa mabao 2:0. Hatima champions League na mapema hivyo ni madhambi makubwa.Vyombo vya habari vya Itali vikinoa shoka la kumfyeka Ancelotti vikimtaja kocha wa zamani wa FC Porto na Chelsea,Jose Mourinho au kocha wa zamani wa taifa wa Itali Marcello Lipi kuwenda kuiokoa AC Milan.Akina Filipo Inzaghi na wenzake walitiwa wote mfukoni na walinzi wa Arsenal.

Mahasimu wao katika premier League-Manchester united nao wakailaza Lyon ya Ufaransa kwa bao 1:0 kwa msaada wa jogoo lao la Ureno-Christiano ronaldo.Hilo lilikua bao la 30 katika mapambano 30 kwa Ronaldo.

FC Barcelona ya Spian iliikomea jana Celtic Glasgow bao 1:0 na kukata tiketi yake ya duru ijayo ya robo-finali.lakini mabingwa hawa wa 1967 wakiwa wakati ule timu ya kwanza ya Uingereza kulinyxanyua kombe la klabu bingwa la Ulaya, waliwatoa jasho muda mrefu wakatalani.

Kwa mwaka wapili mfululizo waskochi celtic wamewasili hatua hii ya timu 16 za mwisho,hatua ambayo hawakuifikia tangu 1989 wakati mwaka jana walitimuliwa na mabingwa AC Milan.

Waturuki jana walisherehekea usiku mzima baada ya klabu yao Fenerbahce kuilaza Sevilla ya Spain na kuingia robo-finali ya champions League .Fenerbahce imekuwa sasa timu yapili ya Uturuki kuwasili robo-finali ya champions League baada ya mabingwa wa zamani wa kombe la UEFA galatasary Istanbul.