Uhalifu
Kongo yawaachilia Wachina waliokamatwa kwa uchimbaji haramu
26 Desemba 2024Matangazo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewaachilia huru raia 14 kati ya 17 wa China waliokamatwa kwa tuhuma za kuendesha mgodi wa dhahabu kinyume cha sheria.
Walikamatwa wiki iliyopita pamoja na wengine kutoka Kongo na Burundi kwa kushindwa kuonyesha nyaraka muhimu wakati wa operesheni dhidi ya uchimbaji haramu wa madini.
Soma pia: Je Ulaya ina nafasi gani katika soko la Cobalt ya Congo?
Gavana wa Mkoa wa Kivu Kusini, Jean-Jacques Purusi Sadiki, alisema alishtushwa na habari za kuachiliwa kwa watu hao, akiongeza kuwa wachimbaji hao wa Kichina walikuwa wanadaiwa dola milioni 10 kama kodi na faini.
Ubalozi wa China haujatoa tamko, huku ubalozi wa Burundi ukisubiri maelezo zaidi kutoka kwa mwakilishi wake Bukavu.