1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini kutoacha mradi wa kinuklia

20 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZM

Beijing:

Balozi wa Korea Kaskazini, Kim Gye-gwan, amesema leo kuwa serikali yake haitaacha miradi yake ya kinuklia kabla ya kupewa zawadi. Miongoni mwa zawadi hizo ni kinu chepesi cha maji na ameiomba Marekani ichukue hatua haraka. Balozi Gye-gwan amesema kuwa wanaambiwa waache kila kitu bila ya kuhakikishiwa usalama wao, manufaa ya kiuchumi, msaada wa nishati na mapatano ya kupatiwa kinu chepesi cha maji kwa wakati unaofaa. Balozi Gye-gwan amesema kuwa Marekani lazima itimize ahadi zake. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kaskazini, Kim Yong-il, amesema kuwa rauni ya tano ya mazungumzo, itakayoanza mwezi wa Novemba mwaka huu, itajishughulisha na „Nipe nikupe.“ Amemaliza kwa kusema kuwa kufikia mapatano ni muhimu lakini muhimu zaidi ni utekelezaji wa mapatano hayo.