SiasaKorea Kusini
Korea Kaskazini na Marekani zaanza luteka ya majini
23 Machi 2023Matangazo
Mazoezi hayo yanafanyika siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.
Jeshi la Korea Kusini limesema takriban wanajeshi 12,000 kutoka nchi hizo mbili watashiriki katika mazoezi hayo, aidha kutakuwa na meli za kivita 30, ndege 70 na magari 50 ya kivita.
Masaa machache baada meli ya kivita kutia nanga, Korea Kaskazini ilifyatua makombora manne kutoka katika pwani yake ya mashariki. Korea Kusini ilisema hatua hiyo inaonesha wazi upinzani wa mazoezi yake na Marekani.