Korea kaskazini yaharibu kinu chake cha kinuklia cha Yongbyong
28 Juni 2008Matangazo
YONGBYON
Rais Goerge W Bush wa Marekani ameiondoa Korea Kaskazini katika orodha yake ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani na pia ametangaza kwamba ataondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
Hatua hiyo imefuatia uamuzi wa kijasiri wa Korea Kaskazini wa kuharibu kinu chake cha Kinuklia cha Yongbyong.Hatua hiyo ya Korea kaskazini imeonekana kama ni ishara ya aina yake iliyoonyesha kujitolea kwa taifa hilo katika kuondokana na silaha za kinuklia.Mtambo huo wa Yongbyong ulikuwa ukitumiwa kutengenezea madini ya Plutonium yanayohitajika katika mpango wa kutengeneza silaha ulionekana kufikia kilele mwezi Oktoba mwaka 2006 baada ya nchi hiyo kufanya majaribio.