1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yajadiliwa.

Halima Nyanza7 Desemba 2010

Mawaziri wa mambo ya nchio za nje wa Marekani, Japan na Korea kusini wamekutana jana kuijadili Korea kaskazini.

https://p.dw.com/p/QRB5
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton.Picha: AP

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Clinton amefungua mkutano aliouita kuwa ni muhimu na mawaziri wenziye kutoka katika nchi za Japan na Korea kusini kujadili vitendo vya uchokozi vilivyofanywa na Korea kaskazini hivi karibuni.

Viongozi hao pia wameishinikiza China na Urusi kutuliza hali ya wasiwasi iliyoko katika eneo la rasi, ambalo China imeonya kuwa itashindikana kuzuilika iwapo halitadhibitiwa ipasavyo.

Novemba 23 mwaka huu, Korea kaskazini ilikishambulia kisiwa cha Yeonpyeong kilichopo Korea kusini, ikiituhumu Seol kwamba inajaribu kuanza tena vita kwa kutumia ujanja mpya.

Südkorea Insel Yeonpyeong Beschuss durch Nordkorea
Kisiwa cha Yeonpyeong, cha Korea kusini kilichoko mpakani na Korea kaskazini ambacho kimeshambuliwa.Picha: AP

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu itachunguza kama shambulio hilo la Korea kuskazini dhidi ya kusini ni uhalifu wa kivita.