SiasaJapan
Korea Kusini: Aliyekuwa Rais akaidi agizo la kuhojiwa
25 Desemba 2024Matangazo
Yoon Suk Yeol leo amekataa kutii wito wa mamlaka ya kupambana na ufisadi nchini humo. Mamlaka hiyo pamoja na waendesha mashtaka, wameanzisha uchunguzi juu ya uamuzi wa ghafla wa Yoon Suk Yeol wa kutangaza sheria hiyo ya kijeshi. Tangazo hilo la sheria ya kijeshi lilipingwa mara moja na wanasiasa wa Korea Kusini. Hatua ya Yoon ya kukaidi mara kwa mara na kushindwa kujitokeza kuhojiwa imezua ukosoaji kutoka kwa upande wa upinzani ambao sasa unatoa wito wa kukamatwa kwake, huku ukieelezea wasiwasi wa uwezekano wa kuharibiwa ushahidi. Wakili anayemshauri Yoon amesema yuko tayari kufika mahakamani kuwasilisha maoni ya mteja wake katika kesi hiyo.