Korea ya Kaskazini yafunga virago
22 Juni 2010Matangazo
Katika mchezo wa jana Jumatatu, Chile iliifunga Uswisi kwa bao 1-0 na Ureno nayo imeitoa Korea ya Kaskazini katika kinyanganyiro hicho cha Kombe la Dunia baada ya kuikandika mabao 7-0.
Katika mechi nyingine,bingwa wa Ulaya Uhispania, hatimae imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini baada ya kuifunga Honduras mabao 2-0.
Sasa, Uhispania inapaswa kuifunga Chile, zitakapokumbana siku ya Ijumaa mjini Pretoria ili iweze kujipatia tikti ya kuingia katika duru ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia.
Timu zilizofanikiwa kusonga mbele katika duru ya pili ni Uholanzi na Brazil. Cameroon na Korea ya Kaskazini zimeshatimuliwa katika duru hii ya kwanza.