1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea ya Kaskazini yaunga mkono mazungumzo ya kinyuklea

27 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFog

PYONGYANG: Korea ya Kaskazini imesema inaunga mkono kuanzishwa tena ile duru ya mazungumzo ya mataifa sita juu ya shauri la kumalizwa miradi yake ya kinyuklea yenye kusababisha ubishi mkubwa kimataifa, aliarifu Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uchina Wang Yi, baada ya kufanya mazungumzo ya upatanishi mjini Pyongyang. Hata hivyo, Waziri huyo wa Uchina, Wang hakuweza kutaja tarehe ya mazungumzo hayo. Kimsingi, Korea ya Kaskazini itayari kukomesha miradi yake ya kinyuklea, ikiwa yatazingatiwa maslahi yake ya usalama. Miongoni mwa mataifa hayo sita ni Korea ya Kusini, Marekani, Urusi na Japan. Mapatano ya mwanzo yalimalizika mwezi wa Agosti bila ya matokeo.