Matangazo
Miongoni mwa yaliyoripotiwa barani Afrika wiki hii ni msako dhidi ya mashoga jijini Daresalam huko Tanzania,Marekani ilitowa tahadhari kwa raia wake walioko katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki huku mashirika mbali mbali ya kutetea haki za binaadamu yakilaani hatua ya kuwaandama mashoga iliyotangazwa katika jiji la Daresalam na mkuu wa mkoa huo,Paul Makonda.Nchini DRC mchakato wa kumchagua mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya upinzani katika uchaguzi wa desemba ndiyo iliyokuwa habari kubwa,wakati kisiwani Madagascar nako taharuki imetanda matokeo ya uchaguzi yakisubiriwa.