1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan

1 Agosti 2011

Karibu Waislamu kote duniani leo wanaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, huku njaa na ukame umetanda hasa huko Somalia na katika maeneo mengine ya Mashariki mwa Afrika na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

https://p.dw.com/p/127Je
Waislamu kote duniani wameuanza mwezi mtukufu wa RamadhanPicha: AP

Ramadhan ni mwezi wa Ibada kwa Waislamu, lakini wakati huohuo kunatolewa miito kwao na kwa wasiokuwa Waislamu kuwafikiria watu wanaosumbuka kwa njaa wakati huu katika maeneo ya Pembe ya Afrika.

Othman Miraji punde hivi amezungumza na Sheikh Sayyid Ahmad Badawy, mwalimu wa mafunzo ya Kiislamu huko Malindi, Kenya, na kwanza alielezea tofauti ya saumu ya Ramadhan na mifungo ya watu wa dini nyingine...

Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Josephat Charo