Kufungua biashara – Jinsi ya kuwa bosi wako mwenyewe!
10 Mei 2012“Ninataka kuanzisha biashara” – Hii ni sentensi ambayo utaisikia mara nyingi zaidi unapowauliza vijana wa Kiafrika kuhusu ndoto zao za baadaye. Lakini mara nyingi vijana hao hawafahamu jinsi ya kutimiza ndoto hiyo na hivyo huanzisha biashara kwa sababu tu ya kukosa ajira. Hivyo wengi wao huishia kufanya kazi katika sekta binafsi na hivyo kuendeleza umaskini.
Mchezo wetu unaoitwa “Kuanzisha biashara” unaeleza kisa cha marafiki watatu Mariam, Abbas na Kossi, ambao wamemaliza shule hivi karibuni na wanakaribia kujiajiri wenyewe. Wasikilizaji watawasindikiza katika safari yao ndefu na kujifunza hatua zote za muhimu zinazohitajika ili kuwa mjasiriamali mzuri. Hatua hizo ni kuanzia kutafuta wazo la biashara linaoonyesha kuleta faida hadi kufahamu jinsi ya kusajili na kugharamia kampuni.
Kisa hiki cha kusisimua kinaambatana na ushauri kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya biashara. Daniel Huba ni mhadhiri kijana katika kitengo cha maendeleo ya biashara katika chuo kikuu cha Inoorero kilichopo Nairobi. Huba anawapa wasikilizaji ushauri muhimu kuhusu kile kinachotakiwa kutiliwa mkazo pale ambapo biashara inaanzishwa na think in terms of opportunity rather than necessity.
Vipindi vya Deutsche Welle “Learning by Ear – Noa Bongo! Jenga Maisha Yako” vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic.