MigogoroBenin
Kundi la kigaidi JNIM ladai kuhusika na shambulio la Benin
11 Januari 2025Matangazo
Kundi linalotajwa kuwa na mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda Afrika Magharibi, JNIM, limedai kuhusika na shambulio lililoua takriban wanajeshi 28 wa Benin.
Shambulio hilo lililofanyika siku ya Jumatano jioni kaskazini mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa Niger na Burkina Faso, limesababisha hisia kali nchini humo.
Siku tatu baada ya shambulio hilo, vyanzo vya kijeshi vimesema idadi huenda ikaongezeka kulingana na hali ya afya ya waliojeruhiwa. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa serikali au jeshi la Benin kuhusu tukio hilo.
Mashambulizi kaskazini mwa Benin yameongezeka katika miaka ya hivi karibuni, huku mamlaka zikiwashutumu wapiganaji wa makundi ya Al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu walioko kwenye nchi jirani.