Kura zaanza kuhesabiwa nchini DRC
29 Novemba 2011Matangazo
Shughuli za kuhesabu kura zimeanza pia mashariki ya nchi hiyo, ambako nako pia hali ya usalama ni ya kuridhisha, baada ya kuripotiwa visa kadhaa vya ukosefu wa usalama jana (28.11.2011) usiku.
Mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo anaeleza hali ilivyo mchana huu mjini Kinshasa.
Pia Saumu Mwasimba amezungumza na makamu kiongozi wa Mashirika ya Kiraia ya Kutetea Haki za Binadamu ya Kivu Kaskazini, Omar Kavota, kuhusiana na matukio ya uvunjwaji wa haki za binaadamu ndani ya siku mbili za upigaji na uhisabuji kura.
Ripoti: Saleh Mwanamilongo
Mahaojiano: Saumu Mwasimba/Omar Kavota
Mhariri: Othman Miraji