Ashley Ngoiri anatajwa kuwa ndiye mkufunzi wa kwanza wa kike wa mchezo wa Majambia nchini Kenya. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 25 amepata fursa ya kuondokana na umaskini kupitia mchezo huo na pia amekabiliana na unyanyasaji wa kijinsia. Sasa anataka kusaidia watu wengine na kutimiza ndoto yake kubwa.