Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia operesheni za amani Jean-Pierre Lacroix amekamilisha ziara yake ya siku tatu huku hali ya kiusalama jimboni Kivu ikiwa imezorota. Ziara hiyo imekuja siku kadhaa kabla baraza la usalama la umoja huo kuongeza muhula wa kikosi cha Monusco nchini Kongo. Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo alituarifu.