1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lahm atafakari kuhusu kustaafu

15 Novemba 2016

Philip Lahm amekataa kuweka wazi iwapo atastaafu soka ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/2Sk6g
Champions League Bayern München vs. PSV Eindhoven
Picha: picture-alliance/dpa/T. Hase

Mchezaji huyo kiungo na kapteni wa Bayern Munich, Philip Lahm ambaye tayari ametundika daluga katika soka la kimataifa, anasalia na mwaka mmoja wa mkataba wake ingawa amesema ukakamavu wake ndio utatoa mwelekeo wa hatima yake.

Kiungo huyo Jumatano hii ameliambia jarida la michezo la Ujerumani 'Sport Bild' kwamba amekuwa akitafakari kuhusu mkakati wake wa kustaafu soka kwa muda mrefu, lakini hakujakuwa na mabadiliko yoyote. 

"Bado nina miezi saba imesalia katika msimu huu ambao, mengi yanaweza kujitokeza. Sitataka kuweka wazi hatma yangu kwa sababu tu ya makombe, bali nitaangalia mwili wangu uko katika hali gani ndipo nitaamua" amesema Lahm.

Lahm ana mkataba na Bayern Munich unaomalizika June 30, 2018. Kando na kucheza miaka miwili kwa mkopo na Stuttgart, Lahm ametumia muda wake mwingi akichezea kikosi hicho kinachotawala Bundesliga.

Alistaafu soka la kimataifa baada ya kufanikiwa kuiongoza Ujerumani kuchukua kombe la dunia, mwaka 2014.

Mwandishi: Lilian Mtono
Mhariri: Gakuba Daniel