1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lavrov ziarani Malta

5 Desemba 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, yuko nchini Malta kwa ajili ya mkutano wa Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano ya Ulaya (OSCE).

https://p.dw.com/p/4nlIk
Sergei Lawrow
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.Picha: Russian Foreign Ministry/Handout via REUTERS

Ikiwa ziara yake ya kwanza kwenye taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu kuanza kwa vita vya Ukraine, Lavrov aliwasili kwenye mji mkuu wa Malta, Valletta, hapo kwa jana kwa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa kigeni wa jumuiya hiyo.

Picha za vidio zilimuonesha waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Urusi akiwasili kwa ndege ya nchi yake, ingawa ndege za Urusi zimepigwa marufuku kwenye anga la Umoja wa Ulaya.

Soma zaidi: Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi yuko ziarani Cairo

Hata hivyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zakharova, amezuiwa kumsindikiza Lavrov, baada ya viza yake kufutwa na Malta muda mfupi kabla ya kuondoka Moscow.