LIBREVILLE: Rais Omar Bongo wa Gabon amewataka waasi wa zamani wa Ivory Coast ...
26 Novemba 2003Matangazo
kurudi kujiunga na serikali yao ya mpito, tangu walipojitoa miezi miwili iliopita, wakilalamika kuwa rais Laurent Gbagbo amekuwa akisumbua juhudi za kuimarisha amani nchini. Bongo alikutana masaa mawili jana na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro ambaye pia ni waziri wa mawasiliano wa serikali ya uwelewano ya Ivory Coast. Mkataba wa amani Januari uliofikiwa kwa juhudi za upatanishi wa Ufaransa, ulipelekea kuundwa serikali ya uelewano, ambayo waasi walijumuishwa nayo.