1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbabe wa kivita wa Libya Khalifa Haftar aenda Urusi

27 Septemba 2023

Mbabe wa kivita mashariki mwa Libya Khalifa Haftar amekwenda Urusi jana Jumanne kwa ajili ya kuzungumzia hali katika taifa hilo lililokumbwa na mafuriko na kuharibiwa na vita.

https://p.dw.com/p/4WqMQ
Flut Libyen Darna
Picha inayoonyesha eneo lililoharibiwa na mafuriko yaliyoikumba Libya hivi karibuni. Hii ni moja ya ajenda zitakazojadiliwa na mafisa hao wawili wanaokutana Moscow.Picha: Halil Fidan//AA/picture alliance

Taarifa ya jeshi lake imesema Haftar alipokelewa na naibu waziri wa ulinzi wa urusi Yunus-Bek Yevkurov, ambaye ni kiongozi wa iliyowahi kuwa jamhuri wa Urusi ya Ingushetia iliyokaliwa na idadi kubwa ya Waislamu.

Taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye Facebook imesema ajenda za mazungumzo hayo zitaangazia hali ilivyo nchini Libya, mahusiano baina ya mataifa hayo na namna ya kuyaimarisha pamoja na masuala yanayogusa maslahi ya pamoja na Urusi na Libya.

Yevkurov amezuru mashariki mwa Libya mara kadhaa kumtembelea Haftar na mara ya mwisho walikutana Septemba 17 katika makao makuu ya jeshi la Haftar, yaliyoko Benghazi.