Lissu atoa wito uchaguzi wa Chadema ufanyike kwa uwazi
2 Januari 2025Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania Bara, alitumia hotuba ya kuukaribisha mwaka 2025 hapo jana, kutaka uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Januari 21 uwe na waangalizi wa ndani na wa kimataifa.
Soma pia: Je, kuna mpasuko ndani ya Chadema?
Lissu aliyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kutangaza nia ya kukitetea kiti chake, akidai kuwa ingawa alikuwa anatamani kuondoka, lakini minyukano iliyopo ndani ya chama imemfanya kubakia.
Uchaguzi mkuu wa mara hii wa Chadema unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, na tayari makundi yanayowaunga mkono wagombea hao wawili yameshajenga kambi zinazotupiana tuhuma nzito nzito, katika kile wachambuzi wa mambo wanachohofia kuwa huenda kikakigawa chama hicho.