1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Mahakama ya Uingereza yamtia hatiani rais wa zamani wa Zambia kwa wizi

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4q

Mahakama ya Uingereza imemtia hatiani rais wa zamani wa Zambia Fredric Chiluba kwa wizi wa dola milioni 46 alipokuwa madarakani.

Jaji Peter Smith wa mahakama hiyo ya mjini London amesema kuwa wazambia watambue sasa kuwa nguo za thamani alizokuwa akivaa Chiluba zilitokana na wizi huo.

Msemaji wa rais huyo wa zamani wa Zambia alisema mjini Lusaka, Chiluba hayatambui na hakubaliani na mamlaka ya kisheria ya mahakama hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa kwa niaba ya mwanasheria wa serikali ya Zambia, ambapo bwana Chiluba hakuwepo kwenye mahakama hiyo kuu ya London wakati hukumu hiyo ikisomwa, na huenda ikapelekea kukamatwa kwa mali zake.