1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Ushirikiano mpya katika sekta ya afya kuwanufaisha masikini

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWm

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na waziri mkuu wa Uingereza bwana Gordon Brown wamefafanua mipango ya kuimarisha huduma za afya kwa manufaa ya nchi masikini duniani. Kansela Merkel na waziri mkuu Brown wamesema hatua za haraka lazima zichukuliwe ili kuyakabili maradhi kama ukimwi,kupunguza vifo vya watoto na vya wanawake katika nchi zinazoendelea.

Viongozi hao wamesema hayo baada ya mazungumzo yao mjini London.

Waziri mkuu Brown amesema kuwa mpango mpya wa kimataifa wa ushirikiano katika mambo ya afya utazinduliwa mapema mwezi ujao kwa ili kuhakikisha kuwa misaada inayotolewa itelenga mahitaji ya afya ya nchi zinazoendelea.