Lusaka. Wanafunzi 42 wafariki katika ajali nchini Zambia.
9 Aprili 2005Matangazo
Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyowakumba wanafunzi wa sekondari nchini Zambia imepanda na kufikia 42 leo na hali za wanafunzi wengine zaidi ya 40 ni mbaya.
Msemaji wa polisi Bibi Brenda Muntemba amesema kuwa hali za majeruhi wengi imezidi kuwa mbaya , kwa sababu Hospitali waliyopelekwa ya kijijini kaskazini mwa Zambia ambako ajali hiyo imetokea jana haina vifaa vya kushughulikia tukio hilo.
Wanafunzi 38 walifariki jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wakati wakirejea nyumbani kutoka shule kwa ajili ya likizo huko Kawambwa. Muntemba amesema kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kukata kona na gari kupinduka mara kadha.