LYON : Ligi ya mabingwa Ulaya
9 Machi 2005Matangazo
Mabingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani , Bundesliga, Werder Bremen wameng’olewa katika kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa barani Ulaya jana usiku. Mabingwa hao wa Bundesliga walipoteza mchezo wa dhidi ya mabingwa wa Ufaransa Olympique Lyon kwa mabao 7- kwa mawili. Werder ilipoteza pia mchezo wa kwanza uliofanyika Bremen Ujerumani kwa mabao 3-0.