MigogoroMashariki ya Kati
Maafisa: Mashambulizi ya Israel yaua watu 28 Gaza
12 Desemba 2024Matangazo
Moja ya mashambulizi hayo yametokea katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, usiku wa kuamkia leo.
Mashambulizi mengine mawili yamesababisha vifo vya wanaume 15, ambao walikuwa sehemu ya walinzi wanaolinda misafara ya malori ya misaada.
Mauaji hayo yamefanyika saa chache baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio la kutaka kusitishwa mara moja na bila masharti mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Wakati huo huo, kundi la wanamgambo la Kipalestina la Hamas limesema limepongeza hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kusitisha mapigano Gaza.
Hamas imesema hatua hiyo itawawezesha raia wa Gaza kupata mara moja huduma muhimu na misaada ya kiutu.