1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChina

Maafisa wa China na Marekani wakutana ili kukuza mahusiano

6 Juni 2023

Vyombo vya habari vya serikali ya Beijing vimeripoti hii leo kuwa maafisa kutoka China na Marekani walikuwa na majadiliano ya wazi, yenye kujenga na yenye manufaa kuhusu kushughulikia vyema tofauti zao

https://p.dw.com/p/4SEuE
China | Daniel Kritenbrink Peking
Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Asia Mashariki na Masuala ya Pasifiki Daniel KristenbrinkPicha: Thomas Peter/REUTERS

Vyombo vya habari vya serikali ya Beijing vimeripoti hii leo kuwa maafisa kutoka China na Marekani walikuwa na majadiliano ya wazi, yenye kujenga na yenye manufaa kuhusu kushughulikia vyema tofauti zao na kukuza mahusiano kati ya mataifa hayo mawili. Jarida la Beijing Daily limebaini kuwa China imetoa msimamo wake madhubuti kuhusu masuala muhimu ikiwemo suala tete la Taiwan, na pande zote mbili wamekubaliana kudumisha mawasiliano. Hapo jana, makamu waziri wa mambo ya nje wa China Ma Zhaoxu alikutana kwa mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Asia Mashariki na Masuala ya Pasifiki Daniel Kristenbrink pamoja na Afisa wa baraza la Usalama wa Kitaifa Sarah Beran. Mahusiano ya China na Marekani yamekuwa yakidorora kwa muda sasa kufuatia tofauti zao za kisiasa, kiusalama na hata kiuchumi.