JangaUfaransa
Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido yafika watu 39
25 Desemba 2024Matangazo
Mamlaka hata hivyo imesema maelfu ya watu huenda wamepoteza maisha kufuatia kimbunga hicho.
Mamlaka imeongeza kuwa shughuli ya kuhesabu watu waliofariki inaweza kukumbwa na changamoto kutokana na baadhi ya watu kuwazika wapendwa haraka kulingana na mafundisho ya kidini, na pia kwa sababu wengi waliofariki walikuwa wahamiaji wasiokuwa na vibali.
Soma pia: Ufaransa yafanya maombolezo ya wahanga wa kimbunga huko Mayotte
Kasi ndogo ya kupeleka misaada visiwani humo imewakasirisha wenyeji wa Mayotte, eneo maskini zaidi lililoko chini ya Ufaransa.
Ama kwa upande wa Msumbiji, nchi hiyo imeripoti vifo vya watu 94 vilivyotokana na kimbunga hicho wakati nchi Jirani ya Malawi ikiripoti vifo 13.